Maonyesho ya wiki ya chakula duniani yazinduliwa mkoani Kagera

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji yashiriki maonyesho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Kagera.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mkuu wa Wilaya Muleba Dkt Abel Nyamahanga amesema Mkoa wa Kagera unakabiliwa na changamoto ya udumavu na kuwataka wadau wa lishe wakiwemo washiriki wa maonyesho hayo kwa ujumla kushirikiana kukabiliana na changamoto hiyo kila mmoja kwa nafasi yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi idara ya uendeshaji kutoka tume ya Taifa ya umwagiliaji Salome Dickson amesema kuwa wamejiandaa kutoa elimu ya kutosha Kwa wakulima juu ya mambo mbalimbali ikiwemo majukumu ya tume kama kusimamia,kuratibu na kuendeleza miundombinu yote ya umwagiliaji nchini.

Pia amewataka wakulima mkoani Kagera na maeneo jirani kutumia fursa ya maonyesho hayo kwa kufika katika banda lao ili kupata elimu na uelewa juu ya kilimo cha umwagiliaji wa kisasa.

Related Posts