TIC YAADHIMISHA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE KWA KUSHIRIKI UPANDAJI MITI JIJINI ARUSHA


IKIWA ni Sehemu ya Ushiriki wa TIC katika tukio la kimkakati la LandRover Festival 2024 na adhimisho la Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa awamu ya kwanza na Mwasisi wa Taifa, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimeshiriki katika Zoezi la Upandaji miti katika eneo la viwanja vya Magereza Kisongo Jijini Arusha leoOktoba14, 2024,
Upandaji Miti ni Sehemu ya Utunzaji wa Mazingira kwa lengo la kujenga na kukuza fursa za Uwekezaji katika mazao mbalimbali ya Misitu na fursa ibukizi ya CARBON CREDIT, tukio hili muhimu limefanyika ikiwa ni sehemu ya kuyaenzi kwa vitendo Maisha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa mhifadhi mahiri wa Mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Upandaji Miti ni sehemu ya Jitihada za Kituo cha Uwekezaji Tanzani (TIC) Kuunga Mkono Jitihada za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara namba moja wa Utunzaji Mazingira na Uhamasishaji Uwekezaji Nchini.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ni kati ya Waratibu na wafadhili wa LandRover Festival 2024 na tumeshiriki kikamilifu kwa kuwa na Banda kubwa linalotumika kutoa Elimu na Kunadi Fursa mbalimbali za Uwekezaji katika Nchi yetu zinazojumuisha Sekta ya Utalii, Kilimo, Madini, Viwanda na Ujenzi wa Nyumba za Bishara Zikiwemo Kumbi kubwa za Mikutano “MICE Tourism facilities”, Kumbi za Sinema, Mahoteli na Nyumba za Kulala Wageni ili kuongeza idadi ya Vitanda na kukabiliana na Ongezeko la idadi ya Watalii linalochagizwa na Program Maalum ya Tanzania – The Royal Tour iliyoasisiwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Tukio la Landrover Festival Banda la TIC ambalo pia ni mahususi kwa ajili ya Mikutano ya Kibiashara “B2B/Speed Networking” limevutia zaidi ya washiriki 300 waliofika kwa nia ya kupata elimu ya Uwekezaji na Utaratibu wa Kusajili miradi ya Uwekezaji na Vivutio vya Kikodi na Visivyo vya Kikodi vinavotolewa na Serikali Kupitia TIC kwa lengo la kupunguza gharama za Mtaji wa Uwekezaji.

Related Posts