Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekutana nchini Luxembourg na kushindwa kuficha tofauti zao kuhusu mzozo unaoendelea mashariki ya kati.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Luxembourg, Xavier Bettel, amesema wazi kwamba Umoja huo sasa unakosa ushawishi na kwamba kuna mgawanyiko mkubwa kati ya mawaziri hao.
Katika majadiliano, baadhi ya mawaziri walilaumu mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, ambapo wanapambana na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.
Uingereza, ikiwakilishwa na waziri wa mambo ya kigeni, David Lammy, ilishiriki katika mkutano huo kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili.
“Usalama wa Uingereza na Ulaya hauwezi kuwa na mgawanyiko, iwe ni kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine au masuala makubwa ya Mashariki ya Kati. Ni muhimu kwa Uingereza na Ulaya kuwa thabiti, Lammy alisisitiza.”
Vikwazo dhidi ya Iran na Moldova
Katika mkutano huo, mawaziri wa Umoja wa Ulaya pia walitangaza vikwazo dhidi ya watu watano na kampuni moja kwa tuhuma za kujaribu kuiyumbisha Moldavia.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Ulaya kupunguza ushawishi wa Urusi barani Ulaya.
Waliowekewa vikwazo ni pamoja na gavana wa mkoa wa Gaga nchini Moldavia, Eugenia Gutful, na maafisa wengine waliohusika na shughuli za watu wanaotaka kujitenga katika eneo hilo.
Soma pia: Rais wa Moldova aishutumu Urusi kupanga njama ya kuuangusha uongozi wake
Aidha, mawaziri hao walitangaza vikwazo dhidi ya naibu waziri wa ulinzi wa Iran, Sayed Hamzeh Ghalandari, na maafisa wa bunge wa Iran.
Vikwazo hivi vinatokana na tuhuma za kushiriki katika kupeleka Urusi droni, makombora, na vifaa vingine vinavyotumika katika vita dhidi ya Ukraine.
Ghalandari na maafisa sita wa bunge wamepigwa marufuku kusafiri katika Umoja wa Ulaya, na mali zao zimeshikwa.
Umoja wa Ulaya pia umetangaza kuzishikilia mali za mashirika ya ndege ya Iran, Mahan na Saha, yaliyotumika kupeleka droni na makombora yaliyotengenezwa na Tehran.