Halmashauri ya mji Geita yaanza kutekeleza agizo la Serikali kutenga Billion 1 za mikopo

Halmashsuri ya Mji Geita Imeanza kutekeleza Maagizo ya Serikali ya kutenga kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 1 kwa robo ya Mwaka wa Fedha za Mikopo za Asilimia 10 ikiwa ni Sehemu ya Maagizo yaliyotolewa na Serikali hivi karibuni.

Akizungumza katika Ufunguzi wa Semina ya kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halamshauri ya Mji Geita Kaimu Mkurugenzi Halmshauri hiyo Bw.Leonard Chacha amewataka Maafisa hao kuhakikisha wanatoa Mikopo hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Serikali bila kuingiza urasimu.

” Kwa kipindi cha Robo tutaona Halmashauri robo hii ambayo tuko nayo tumetenga Bilioni Moja na Hii Bilioni moja lazima iishe yaani lazima iishe mlisikia bilioni moja muda tulip nao na kasi tunayo enda nayo lazima iendane na bilioni moja kwahiyo tageti sisi kama Halmashauri lazima tuifikie , ” Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Geita Bw. Chacha.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Geita Last Lingston amesema toka mikopo imesitishwa tayari Halmashauri ya Mji wa Geita imekwisha kurejesha Fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 fedha ambazo zilikuwa zimeachwa kwenye vikundi.

” Zimefanyika Jitihada kubwa sana Jitihada Mbalimbali za Kimarudhiano lakini pia za hatua nyingine ambayo inalenga kabisa kuwa mikopo inalejeshwa kwa Mfano kwa halmashauri ya Mji wa Geita tangu mikopo imesitishwa April 2023 mpaka sasa zimelejeshwa takribani shilingi Bilioni 2 .5 kutoka kwenye vikundi ambavyo vilikuwa vinadaiwa , ” Afisa Maendeleo Mkoa wa Geita , Last Lingston

Naye Mariam John ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Geita amewataka vijana ambao wamekuwa na changamoto ya kurudisha fedha kuweka Jitihada katika kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo ambayo waraondokana na suala mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira.

Related Posts