Mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge waagwa nyumbani kwake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, leo Oktoba 15,2024 amewaongoza familia na waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge nyumbani kwake Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Mbuge unatarajiwa kuagwa kijeshi kesho Oktoba 16 Oktoba 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baada ya taratibu za kuagwa kijeshi kukamilika, Mwili huo utasafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika Oktoba 17, 2024.

Meja Jenerali Mstaafu Mbuge alifariki alfajiri ya Oktoba 12,2024 akiwa nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Related Posts