Taifa Stars hoi nyumbani – Mtanzania

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 2-0 na DR Congo katika mchezo wa kundi H wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya (AFCON), uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mabao ya DR Congo yamefungwa na Meschack Elia.

Mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana wiki iliyopita Stars ilifungwa 1-0 jijini Kinshasa baada ya Clement Mzize kujifunga.

Ushindi huo unaifanya Congo kufikisha alama 12 na kukata tiketi ya AFCON itakayofanyika mwakani nchini Morocco, huku ikiwa na mechi mbili mkononi

Related Posts