Kiwanda cha Saruji ya Mbeya kufanyiwa maboresho ,Tanga kujengwa kiwanda kipya

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akizungumza kuhusiana na Uwekezaji wa  Maboresho na Ujenzi wa Kiwanda Tanga ,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya AMANSOS  Ahmed Mhada akizungumza kuhusiana  na dhamira ya kufanya uwekezaji katika viwanda vya Saruji,Mbeya na Tanga.

*Msajili wa Hazina asema ni mageuzi ya uwekezaji chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SERIKALI na Kampuni ya Saruji ya Mbeya inayojulikana na chapa yake ya Tembo ambayo pia ni kampuni tanzu ya Amsons wanatarajia kufanya upanuzi wa Kiwanda cha Saruji Mbeya na kujenga kiwanda kipya cha Saruji mkoani Tanga.

Upanuzi wa Kiwanda cha Mbeya na kujenga kiwanda kipya Tanga utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 320.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema kuwa uwezo kiwanda cha Mbeya kuzalisha Tani 1000 kwa usiku hivyo uwekezaji huo utaongeza Tani 5000 kwa siku na kiwanda kitajengwa mkoani Tanga kitazalisha Tani 5000 kwa siku na kufanya uzalishaji huo kuwa Tani 10000 kwa siku.

Mchechu amesema kuwa uwekezaji huo unatokana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini.

Amesema kuwa Serikali ni Mwanahisa mweza wa Amsons ya Kampuni ya Saruji Mbeya kwa miaka 15 ilikuwa haijatoa gawio kwa Serikali ambapo mwaka jana ilitoa gawio la Sh.Bilioni Tatu hivyo itaendelea kutoa gawio.

Aidha amesema katika uwekezaji huo serikali inakwenda kupata faida ya kodi pamoja na ajira kwa watanzania.

Amesema uzalishaji huo saruji itakayozalishwa itapata masoko katika nchi ya Congo baada ya kuona kuwa na soko ya Saruji.

Amesema maboresho na ujenzi wa kiwanda kipya cha Tanga utafanyika katika kipindi miaka miwili hadi mitatu.

Mkurugenzi wa Fedha wa AMASONS Ahmed Mhada amesema uwekezaji huo ni kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya saruji nchini.

Amesema kuwa katika uzalishaji huo watakwenda kuongeza gawio la serikali pamoja na kodi zitazotokana na uwekezaji.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akiwa na Wakurugenzi  Kampuni ya Saruji ya Mbeya inayojulikana na chapa yake ya Tembo ambayo pia ni kampuni tanzu ya Amsons jijini Dar es Salaam.

Related Posts