MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye,akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye,akishuhudia kiapo cha utii cha vijana wa mafunzo ya JKT kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Gwaride la Heshima la Vijana wa kujitolea likipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye (hayupo pichani) kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’,katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Jacob John Mkunda,Mkuu wa Tawi la Logistiki na Uhandisi Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Hawa Kodi,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Kamanda wa Kikosi cha Jeshi cha 825, Luteni Kanali Patrick Ndwenya,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Na.Alex Sonna-KASULU
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ,amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutumia ujuzi waliopata kujiajiri kwa kuwa Tanzania ina kazi nyingi za kufanya.
Mhe.Andengenye,ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea ‘Operesheni ya Miaka 60 ya JKT’, katika kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Mhe.Andengenye,amesema kuwa sio dhambi kuajiriwa lakini tumieni ujuzi kupata kazi kwa sababu kazi wakati mwingine inalipa zaidi ya ajira.
Aidha amewasihi kutumia ujuzi wa kufuga nyuki kazi ambayo ni rahisi na kilimo cha mazao ya bustani.
“Ukitaka kuanza kufuga nyuki hulazimki kwenda benki kukopa fedha kwani wa kuanzia unaweza kutumia mizinga ya asili unayoweza kuchonga kwa mikono,” amesema Mhe.Andengenye
Pia amewataka vijana hao kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yaliyo kinyume na mila na utamaduni wa Watanzania.
Mhe.Andengenye, amesema kuwa Serikali ilitunga Sheria ya Kudhibiti Maudhui Mtandaoni ambapo watakapopatikana na maudhui ambayo ni kinyume na mila na utamaduni, hatua kali za sheria zitacjhukuliwa dhidi yao.
“Natumia fursa hii kuwaasa kuwa hatutakuwa na wasaa mwingine tutakapokuta wewe umeingia kwenye makundi yasiyofaa ambayo siyo yale uliofundishwa hapa (jeshini) ukaingia katika mitandao ya hatakuwa na saa nyingine ya kutoa wasia wakati watakapofanya mambo ya hovyo, bali watawachukulia hatua za kisheria mara moja,”amesema.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Jacob John Mkunda,Mkuu wa Tawi la Logistiki na Uhandisi Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Hawa Kodi amewataka vijana hao kutumia jukwaa hilo kuwaelimisha wengine kwa vitendo kuwa wao ni wazalendo.
“Niwatake kuzingatia na kuheshimu maamuuzi yenu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejitendea haki wenyewe na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na jamii mliyotoka kwa ujumla,”amesema Meja Jenerali Hawa
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji mawazo ya muasisi wa Taifa, Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere katika uanzishwaji wa JKT.
”Naamini kuwa mafunzo haya mliyoyapata mmekuwa tayari kulitumikia na kulilinda taifa letu popote mtakapokuwa kwani mmefahamu dhana ya uzalendo, umoja, mshikamano, ukakamavu na kujiami, mnapaswa kutumia elimu hii katika kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria na taratibu za nchi. Hivyo nendeni mkaishi kiapo chenu.”amesema Brigedia Jenerali Mabena
Hata hivyo Brigedia Jenerali Mabena amewataka vijana hao kutunza afya zao kwani ndio msingi na mtaji wao mkubwa na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, ulevi, utumiaji wa dawa za kulevya, ulaji wa vyakula au utumiaji wa vinywaji vyenye kuhatarisha afya zao.
Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amewaomba vijana hao kwenda kuwaelimisha wazazi na walezi ambao bado wana ukakasi wa kutowaruhusu vijana wao kwenda kujitolea.
“Basi ni vyema wazazi wakawaruhusu vijana wao kuja kujitolea ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata maarifa pamoja na elimu ya ujasilia mali na wawe tayari kulitumikia Taifa lao pindi wanapohitajika,”amesema
Awali Kamanda wa Kikosi cha Jeshi cha 825, Luteni Kanali Patrick Ndwenya, amewaasa vijana hao kwenda kuyaishi mambo yote, waliofundishwa ndani ya wiki 16 waende kuyaishi kwa vitendo katika kipindi chote cha mkataba wa Jeshi na baada.
“Muendelee kuwa na nidhamu na kuepuka matumizi mabaya ya mtandao ya jamii kuepuka ushabiki wa kisiasa, vikundi viovu,ulevi, ngono matumizi ya dawa za kulevya,”amesema Luteni Kanali Ndwenya.