MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua ofisi ya walipa kodi binafsi na wenye hadhi ya juu 158 ilikuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda alizindua ofisi hiyo dar es salaam jana.
“Muunganiko huu na matoke haya ni kutokana na muundo mpya uliotengenezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan,ofisi hii itakuwa ikihudumia makundi manne ambayo ni wamiliki wa makampuni makubwa yanayozalisha zaidi ya Sh. 20 bilioni kwa mwaka, wamiliki wa hisa zenye thamani ya Sh. 2.5 bilioni kwa mwaka,wale wote wenye ubia kwenye makampuni zinazozalisha zaidi ya Sh. 20 bilioni, viongozi wa mihimili mitatu pamoja na taasisi wote watahudumiwa na ofisi hii na ni 30% tu ya mapato watakayochangia,” alisema Mwenda.
Mwenda alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na makundi hayo kwani kushindwa kuyapa huduma stahiki kutasababisha serikali kupoteza mapato na kufanya uchumi wa nchi kushuka.
Alisema Mamlaka imeanza na idadi hiyo kwani ndio waliokidhi vigezo vya kuhudumiwa katika ofisi hiyo.
“Katika makundi yaliyoainishwa walipaji kodi binafsi waliokidhi vigezo na kupata sifa ni 111 huku viongozi kutoka mihimili mitatu na taasisi wakiwa 47 hivyo ni lazima watu hawa tuwenao katibu ilikuwapa elimu zaidi ili waweze kulipa kile wanachostahili,”alisema Mkenda.
Alisema mamlaka inahitaji kuweka na kuleta usawa katika usimamizi na ulipaji wa kodi kwani watu hawa walikuwa wanalipa kodi lakini si kwa ushahihi sababu makundi waliyokuwepo hayakuwa sahihi pia hata huduma walizokuwa wakioewa huko hazikuwa rafiki kwani kuna watu walikuwa kundi la walipa kodi wakubwa, wakati na walipa kodi wadogo sasa tunawaleta pamoja ilikuweza kutafasiri sheria za kodi.
Naibu Kamishina Mkuu wa mamlaka hiyo,Mcha Hassan alisema ufunguzi wa ofisi hiyo ni kuongeza huduma na kuongeza ufanisi wa kazi ilikusaidia kuwatambua walipa kodi wote na nakufahamu zaidi namna ya ulipaji,ili kuongeza uweledi wa ukusanyaji mapato na kuongeza walipa kodi kwa hiari na kuwahudumia bila changamoto.