Kongamano la vijana na Tanzania kukusanya maelfu ya Vijana Mbeya

Zaidi ya Vijana 1000 kutoka mikoa pamoja na wilaya za nyanda za juu kusini pamoja na viongozi mbalimbali wanatarajia kukutana katika kongamano kubwa linalojulikana kama VIJANA NA TANZANIA yenye lengo la kukutanisha vijana na kutoa fursa adhimu kwa vijana bila kujali chama ama dini na kujikita katika mijadala endelevu , kubaini mambo chanya ambayo yanaweza kufanyika kwaajili ya masilahi ya nchi.

Kongamano hilo kubwa Linatarajia kufanyika tarehe 20 oktoba siku ya jumapili jijini Mbeya kwaajili ya kongamano hilo

Akizungumza leo na waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea jijini Mbeya Mratibu wa Kongamano hilo la VIJANA NA TANZANIA Lazaro Nyarandu amesema vijana wote kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini wanaalikwa kushiriki kongamano hilo na kwamba itikadi ya vyama za kisiasa havitakiwi na sio kigezo cha kushiriki

“Siku ya jumapili ya tarehe 20 oktoba mara baada ya ibada tutakusanyika kwaajili ya kongamano la vijana na Tanzania , na vijana watakusanyika mbeya vijana wa aina zote kujadiliana kile ambacho wanahisi wanaweza kufanyia nchii hii “ amesema Nyarandu

Lazaro Nyarandu amesema baada ya kongamano hilo kufanyika Mbeya utaratibu mzuri utapangwa kwaajili ua kutoa fursa ya kongamano hilo kufanyika mikoa mbalimbali .

“Baada ya mbeya tutaanza sasa kwenda mkoa baada ya mkoa na tayari tumekwisha alikwa na baadhi ya mikoa nadhani kila baada ya mkutano wa kongamano tutapiga kura kwa pamoja ni mkoa gani tunapaswa kuelekea “

 

 

Related Posts