MAAFISA WA OYA KIZIMBANI KWA MAUAJI YA MJASIRIAMALI

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
Wafanyakazi wanne wa Taasisi ya Mikopo almaarufu kwa jina la OYA leo tarehe 16 Oktoba ,2024 wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji ya kukusudia na kumuua Juma Said Seif (45),mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi Mkoani Pwani Oktoba 7,2024
Akisoma shitaka hilo Wakili wa Serikali Monica Mwela mbele ya Hakimu Mkaazi Muandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Emmaeli Lukumai, amesema kuwa kesi hiyo yenye namba 29566 2024 ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza.
Aidha Wakili wa Serikali Mwela amewataja watuhumiwa haokuwa ni Dastan John Charles (23)mkaazi wa Kilangalanga Mlandizi,Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi,
Christopher John Charles (23) mkaazi wa Kilangalanga na Emmanuel Joshua Olala(24) mkaazi wa Kilangalanga Mlandizi Kibaha Vijijini.
Baada ya kusikiliza shitaka hilo la mauaji,Mhe. Hakimu Mkazi Muandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Lukumai amesema kuwa kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia ambayo imefikishwa kwa mara ya kwanza ushahidi bado haujakamilika hivyo kesi hiyo itasomwa tena Oktoba 30 2024 huku watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.
Aidha watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.

Related Posts