Watumishi waaswa Ulevi na Rushwa,enendeni kwa maadili kazini

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya 80 ambao wameajiriwa hivi karibuni ikiwa ni Mpango unaoandaliwa na Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu katika kuwaandaa waajiriwa wapya kuendana na Misingi ya Maadili ya Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma.

Akifungua Mafunzo hayo huku akimwakilisha Katibu Mkuu,Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu,Separatus Fella amewataka watumishi hao wapya kujiepusha na masuala ya kupokea rushwa na Tabia Za Kilevi ambazo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika jijini Dodoma huku mada mbalimbali ikiwemo elimu ya afya,elimu ya ustaafu,utoaji huduma na muundo wa Serikali na jinsi inavyofanya kazi kufikisha huduma kwa wananchi.

Related Posts