VYUO VIKUU VYASHAURIWA KUWEKEZA KWA VIJANA

Vyuo vikuu hapa nchini vimeshauliwa  kuwekeza kwa vijana  kwa kuwapatia mitaji  wakiwa bado wanafunzi  ili waweze kuendeleza mawazo ambayo wanayo  ili  kujiari  na kupunguza  wimbi la  kukosekana kwa ajira pindi wamalizapo masomo pia kuweza kuwaajili vijana wenzao. 

Hayo yamebainishwa na umoja  wa wanafunzi ambao walisha wahi kusoma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ikiwa na lengo la kukumbushana mambo mbalimbali ambapo wamevishauri vyuo vikuu hapa nchini kuona namna yakuwasaidia wahitimu wao mitaji ili waweze kujiajiri na kuacha kusubiri kuajiriwa na kuyafanyia kazi mawazo yao waliyotoka nayo Chuo pia kuwapatia ajira vijana wengine.

Aidha, wameuomba uongozi wa  SUA kuwekeza zaidi kwa kutoa elimu ya vitendo kwa wanafunzi ili waweze kupata ujuzi wakutosha.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo  Prof, Raphael Chibunda akaeleza lengo la kukutana na umoja wa wanafunzi ambao walishawahi kusoma kusoma Chuo hicho.

Prof, Chibunda amesema kuwa, Chuo kimeandaa mazingira wezeshi ambayo yatamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri ambapo pia ameishukuru serikali kwa kuendelea  kutoa fedha kiasi cha shilingi takribani bil 70 kwa kuwekeza katika miundombinu.

Naye  Mratibu wa Majalisi wa SUA,  Prof. Jonathan Mbwambo akaeleza  kwenda kuufanyia kazi  ushauri huo uliotolewa na umoja wa wanafunzi hao na kwamba umoja huo utakuwa chachu ya kuimalisha na kuboresha maendeleo ya Chuo hicho.

Related Posts