Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu ya mahudhiro katika msiba wa aliyekuwa Meja Jenerali wa Jeshi wa Wananchi(JWTZ), Charlse Mbunge.
Na mwandishi wetu……………..
Mwili wa aliyekuwa Meja Jenerali wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Charles Mbuge umeagwa leo katika hospitali kuu ya JWTZ jijini Dar es salaam na kusafirishwa kuelekea kijijini kwake Kiabakari, Butiama, ambako unatarajia kuzikwa kesho tarehe 17 oktoba 2024, kitongoji cha Kyabakari, wilaya ya Butiama Mkoani Mara
Meja Jenerali Mbuge alifariki tarehe 12 Oktoba 2024, nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.