Balozi wa bidhaa za taulo za (Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu “Lulu” akikabidhi taulo za taulo (Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex) kwa mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro kulia ni Dkt. Idda Luhanga Mkurugenzi wa Premature Babies Organization.
BALOZI wa bidhaa za taulo za Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu “Lulu” amesema bidhaa hizo zina ubora wa hali ya juu na zinafaa kutumiwa na akina mama mara baada ya kujifungua watoto na nyakati zingine zote kwani zinawafanya kuwa wakavu na salama zaidi
Amesema kama vile bidhaa ya Unisex Adult Diaper hii ni suluhisho la ukavu baada ya kujifungua na inaweza kutumiwa na akina mama wote mara baada ya kujifungua kwani ina uwezo na ukavu mara dufu ambapo inafanya kazi nzuri ya ufyonzaji thabiti, kuzuia kuvuja, ulinzi wa muda mrefu na ni mbadala wa (Maternity Pad) .
Elizabeth Michael ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha mradi wa “Diaper Care” ulioanza tarehe29/04/2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke. Mradi ambao una lengo la kumuelimisha mama juu ya matumizi ya taulo za wakubwa (Adult Diapers) kama mbadala wa pedi za uzazi(Maternity Pads)hasa baada ya kujifungua.
Kampuni ya DRAFCO GROUP LTD inahusika na utengenezaji na usambazaji wa taulo (Baby and Adult Diapers) za BABY CHEEKY, CUIDADO na PINOTEX kwa ajili ya matumizi ya watoto wadogo pamoja na akina mama watu wakubwa hapa nchini Tanzania imeamua kutoa elimu hiyo na msaada wa taulo kwa akina mama wanaojifungua na watoto katika hospitali ya rufaa ya Temeke ili kuwapa uelewa wa namna ya kutumia taulo hizo kuwasaidia gharama za uzazi ikiwa ni pamoja na kuwapa furaha wakati wote watumiapo taulo hizo.
Kampuni hii ikiwa chini ya Balozi wake Elizabeth Michael (Lulu) ndiyo waliowezesha mradi huu kwa kugharamia utoaji elimu, misaada kwa wahitaji na kuhakikisha usambazaji na upatikanaji wa taulo hizi unawafikia walengwa na wahitaji nchi nzima.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro ameipongeza kampuni ya DRAFCO GROUP LTD kwa kutoa elimu pamoja na kugawa taulo za watoto na wanawake kwa wahitaji katika hospitali ya Temeke zenye thamani ya shilingi milioni 16.
“Tunashukuru kwa kuwa tumepewa Diaper kwa ajili ya watoto wachanaga na watu wazima jambo hili mlilofanya ni jambo la kujitolea na ni sadaka”,amesema Dr. Kimaro.
Amesema Serikali inahimiza watu binafsi mashirika na makampuni kusaidia ili kuhakikisha sekta ya afya inaimarika na kugusa maisha ya watu.
Amesema ugawaji wa tauli hizo umesaidia wahitaji wengi lakini umechangia katika sekta ya afya kwenye kuboresha afya za wananchi.
Ameongeza kuwa siku tano za kazi ya kutoa elimu iliyofanyika hospital hapo wameweza kuwafiki akina mama 1500 ambapo watu hao nao wanaweza kupeleka elimu kwa wengine.
“Tunaamini watu zaid ya 15000 watakuwa wamepata elimu kuhusu hizi bidhaa kazi kubwa mmeifanya na sisi tutaendelea kuunga mkono juhudi zenu kwa kufanya tafiti katika hizi bidhaa za taulo za wakubwa”,amesema.
Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro akionesha moja ya picha inayoonesha mtoto njiti.
Dkt. Idda Luhanga Mkurugenzi wa Premature Babies Organization akizungumza wakati wa makabidhiano hayo.