Na Oscar Assenga,PANGANI
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amesema kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ili upate viongozi lazima ufanye uchaguzi huku akiwataka wananchi kujiandikikisha kwenye daftari la kupiga kura ili kutimiza haki yao ya msingi.
Aweso ambaye ni Waziri wa Maji aliyasema hayo leo mara baada ya kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura katika Kijiji alichozaliwa cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani huku akieleza kwamba ni muhimu wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuwachagua viongozi wanakaowaletea maendeleo.
Alisema kwamba ni muhimu wananchi wakatumia muda uliowekwa kwa ajili ya kujiandikisha na ili waweze kupata viongozi ambao wanawataka lakini wakaowaleta maendeleo ikiwemo kuwasikiliza na kushirikiana nao katika kuleta maendeleo kwenye kijiji chao.
“Leo nimejiandikisha kwenye kijiji changu ili apate haki ya msingi kupata kiongozi anayemtaka ambaye atashirikiana na wenzine kuleta amendeleo nito wito wanachi Pangani na watanzania tujitokeza kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi ambao wanashirikiana na Rais katika kuleta maendelelo katika vijiji vyetu”Alisema
Alisema kwamba hiyo ndio ngazi ya msingi hasa kwenye vijiji na vitongoji wanajenga msingi kuhakikisha maendeleo katika ngazi ya vitongoji mpaka vijiji yanakwenda vizuri na wasipate nafasi kulalamika .
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya alisema kwamba zoezi la kujiandikisha kwenye wilaya hiyo lipo vizuri limefikia asilimia 60 ndani ya siku sita za uandikishaji .
“Tunaamini mpaka zoezi hili litakapofika mwisho Octoba 21 mwaka huu tutakuwa tumevuta zaidi ya asilimia 100 ya lengo ambalo tumejiwekea kama wilaya”Alisema
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashsri ya Pangani Akida Bahorera aliwataka vijana watumie fursa ya kujiandikisha pamoja na kujitokeza kwa wingi wakati wa kuchukua fomu ili waweze kugombea nafasi mbalimbali.