PROF. SEDOYEKA MKUU WA CHUO CHA IAA AFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imemfikisha mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma Mkuu wa chuo cha Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamin Sedoyeka kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumpandisha cheo Afisa Rasilimaliwatu II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu bila kuwa na sifa.

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni kuingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza katika kampasi ya Babati kwa kuifuta bila kufuata utaratibu na kufanya uhamisho wa ndani wa mtumishi Afisa Ugavi kutoka kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwenda Idara ya Maktaba tofauti na sifa za kitaaluma za mtumishi.

Akiwasilisha mashtaka mbele ya Baraza tarehe 16 oktoba, 2024 Wakili Mkuu wa Serikali Bi Emma Gelani alilieleza Baraza kuwa mlalamikiwa anakabiliwa na mashtaka manne na ameshindwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) 6(1)(c) na 12(1)(c) vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Mlalamikiwa wakati akitekeleza majukumu yake ya uongozi pasipo kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma alimpandisha cheo Bw. Hakimu Ndatama kutoka Afisa Rasilimali II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu kabla ya kukamilika kwa uhamisho wa mtumishi.”

Bw. Ndatama ambaye ni mmoja kati ya mashahidi wanne waliotoa ushaidi wao mbele ya Baraza alikiri kuwa tarehe 13.5.2023 alipandishwa cheo kutoka Afisa Rasilimaliwatu II kuwa Mkuu wa sehemu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha kabla ya taratibu za uhamisho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii hazijakamilika.

Kuhusu suala la zabuni, Bi Gelani alieleza kuwa mlalamikiwa aliingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza na kuifuta kinyume kifungu cha 59(2) cha Sheriai ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410.

“Kitendo hicho Mhe. Mwenyekiti ni kinyume na kifungu cha 6(1)(c) cha Sheria ya Maadili kinachomtaka kiongozi wa Umma kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria za nchi,”alisema.

Ilidaiwa mbele ya Baraza kuwa Prof. Sedoyeka alifuta zabuni kwa madai kuwa gharama ilikuwa kubwa kuliko bajeti ya taasisi ya shilingi bilioni 1.274

Shahidi wa kwanza katika lalamiko hilo Bw. Ramadhani Mwanang’waka ambaye ni Afisa wa Sekretarieti ya Maadili alisema kuwa katika uchunguzi wao walibaini kuwa kampuni mbalimbali ziliomba zabuni hiyo.

“Niliporipoti Maktaba nilipangiwa kukaa mapokezi kukagua wanafunzi wanaoingia na kutoka ndani ya Maktaba.

Bw. Robert ni Afisa ugavi daraja la I ambaye ni Certified Procurement and Supply Professional (CPSP).

Mlalamikiwa ameyakana mashtaka yote manne na tarehe 17.10.2024 anatarajia kuwasilisha utetezi wake mbele ya Baraza.

Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma linasikiliza lalamiko hilo chini ya Mwenyekiti Mhe. Jaji (Mst.) Rose Teemba na wajumbe wa Baraza Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi.

Related Posts