WAZIRI MHAGAMA KUSHUGHULIKIA HOJA ZA WAUGUZI.

Na WAF, DODOMA

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Oktoba 17, 2024 amekutana na Uongozi wa Chama cha Wauguzi na Ukunga Tanzania (TANNA) na kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za wauguzi zilizo jitokeza wakati wa mkutano wa mwaka uliofanyika 12 Mei, 2024 ili kuongeza ubora wa Huduma kwa wananchi.

Mhe. Mhagama amesema kuwa anatambua mchango na kazi kubwa inayofanywa na wauguzi na wakunga katika sekta ya afya hivyo anawapongeza kwa kazi nzuri inayofanyika katika kuwahudumia wananchi

Amesema moja ya jukumu kubwa analofanyia kazi kwa sasa ni kuhakikisha wauguzi na wakunga wanapandishwa madaraja kama ilivyo kwa kada zingine.

“Wakati tunafanyia kazi changamoto zenu tusaidieni kusimamia maadli kwa wauguzi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi”, ametoa rai Mhe.Mhagama

Amesema serikali kupitia wizara ya Afya inafanya kazi kuhakikisha inatatua changamoto wanazokabiliana nazo wauguzi na wakunga hivyo waendelee kuchapa kazi kwa kufata miiko na maadili ya taaluma wanapo wahudumia wananchi

Kwa upande wake rais wa Chama cha Wauguzi na Ukunga Tanzania ( TANNA), Alexender Baluhya amesema kuwa wauguzi na wakunga wanaimani na serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani kuwa ni sikivu na itatatua changamoto zao kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi wao

Amefafanua kuwa lengo la kukutana na Mhe.Mhagama ni kufatilia utekelezaji wa hoja za wauguzi zilizotolewa katika mkutano wa mwaka uliofanyika pale Mkoani Tanga- na hoja hizo ikiwemo kupandishwa madaraja.






Related Posts