Tanzania yafungua milango katika sekta mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya kuku na ndege wafugwao:Waziri Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa ujio wa Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao kwa Nchi za Kusini mwa Afrika unadhihirisha  namna Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt.  Samia ilivyokuwa na mahusiano mazuri ambayo yamefungua milango katika sekta mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya kuku na ndege wafugwao.

 

Amesema hayo leo Oktoba 16, 2024 jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao Kusini mwa Afrika.

 

Aidha ametaja faida za ufugaji kuku na ndege wafugwao kuwa ni pamoja na kuchangia usalama wa chakula na kuongeza pato la Taifa kikanda na kimataifa.

 

Amesema kuwa asilimia 55 ya kaya nchini na katika nchi mbalimbali ni ufugaji unaofanywa zaidi na wanawake na vijana na kuwa Tanzania ina kuku milioni 103.1 wakiwemo kuku wa asili na kisasa.

 

Kupitia Jukwaa hilo, Dkt. Biteko ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzisha mashamba ya kuku wazazi kwa ajili ya kuzalisha vifaranga, kuanzisha vituo vya kisasa, maabara pamoja na kuwekeza katika machinjio ya kisasa ya kuku.

 

Dkt. Biteko ametoa maagizo mengine ikiwemo “ Wizara iweke pia mfumo wa mnyororo baridi wa usambazaji wa kuku, iwekeze pia katika vizimba, chakula cha kuku na ianzishe viwanda vya kusindika vyakula vya kuku ili vipatikane ndani ya nchi na sio kutumia fedha za kigeni kuagiza nje,”

 

Ametoa wito kwa wadau wote wa ufugaji wa kuku kuendelea  kushirikiana na Serikali kutekeleza majukumu yao kwa kuwa Serikali  imetoa fursa kwa kila mmoja kuweza kujishughukisha na kujiongezea kipato.

 

Fauka ya hayo, Dkt. Biteko ameikaribisha sekta binafsi kushiriki katika tasnia hiyo ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi huku akiwataka watafiti kushirikiana na Serikali.

 

AGRA uliofanyika Dar es alaam na kuongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia ambapo AGRA walielezwa juu ya kuipa kipaumbele sekta ya ufugaji wa kuku kwa kuwa nchini Tanzania familia nyingi zinafuga kuku

“ Tunawashukuru AGRA na Food Alliance kwa kutukubalia na ndio maana leo jukwaa la kwanza limefanyika hapa Tanzania na kutoa fursa kwa wafugaji wetu kujifunza na kujenga mahusiano,” amesema Mhe. Ulega.

Amebainisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa ifikapo 2030 kuku watachangia asalimia 41 ya protini na kuwa watafiti nchini washirikiane na Serikali wanapotoa matokeo ili kutoleta taharuki kwa jamii kupitia matokeo ya tafiti zao.

Related Posts