Kampuni ya michezo ya kubashiri inayokua kwa kasi nchini, LEONBET, imeongeza ladha ya burudani kwa wateja wake kwa kuwazawadia tiketi za VIP kuiona mechi ya Simba na Yanga kupitia kampeni ya kampeni ya Bata La Derby.
Washindi hao wataona mechi hiyo ya ligi kuu ya Tanzania Bara Jumamosi, Oktoba 19, 2024 kuanzia saa 11 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Afisa huduma kwa wateja wa LEONBET, Jacqueline Jonas alisema kuwa mbali ya tiketi ya VIP A, pia washindi hao watakwenda uwanjani kwa usafiri wa kisasa wa kwenda na kurudi, kula bata la kibabe na chakula na vinywaji vya kipekee, na vile kupata fursa ya kukutana na nyota wa comedy nchini Tanzania kabla ya mechi.
“Simba La Mikeka hajawahi kuwa na shoo mbovu. Tuna furaha kubwa kuwapa wateja wetu washindi uzoefu wa kipekee wa mechi hii ya kihistoria.
Hii ni sehemu ya kujitolea kwetu kwa kuwapa wateja wetu burudani bora na ofa za kuvutia,” alisema Jacqueline.
Jacqueline aliongeza kuwa kampeni hii ni mwanzo tu kwani LEONBET ina mipango kabambe zaidi kwa wateja wake, ikiwemo ofa maalum ya Sh 2,000 bure kwa kila mteja mpya anayejisajili na LEONBET.
Alisema kuwa LEONBET imeendelea kuiteka soko la michezo ya kubashiri nchini Tanzania, na wateja wake wanafaidika na huduma bora na zawadi za kuvutia.
LEONBET ni kampuni ya michezo ya kubashiri inayojikita katika kutoa uzoefu wa kipekee kwa wateja wake kwa kupitia michezo ya kubashiri mtandaoni na michezo ya kasino.
Kampuni hii imejidhatiti katika kutoa burudani bora na inazidi kushika kasi katika soko la Tanzania.
Kwa maelezo zaidi na kujiunga na LEONBET, Tembelea: www.leonbet.co.tz..