Na Mwandishi Wetu,Bukoba
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato amesema kuwa wananchi watumie haki yao ya kupiga kura kuchagua viongozi katika uchaguzi wa SerikalI za Mitaa
Byabato ameyasema hayo wakati alipokweda kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Migera Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba, Leo tarehe 18 Oktoba, 2024.
Amesema kuwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika uchaguzi wa serikali bila kujiandikisha huwezi kupiga kura ambapo ni kupoteza haki ya kuchagua viongozi.
Aidha amewataka kila mtu kumhamsisha mwenzake ambaye hajajiandikisha ili kila mtu aweze kushiriki uchaguzi huo.
Byabato amesema kuwa katika uchaguzi huo viongozi wataochaguliwa watatumikia miaka mitano hivyo kila mtu ajindikishe ili wapigiwe kura.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Migera Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba, Leo tarehe 18 Oktoba, 2024.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati alipokwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Migera Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba, Leo tarehe 18 Oktoba, 2024.