MBUNGE UMMY APITA VIJIWENI KUHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA NA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu leo Octoba 18 mwaka 2024 ametembelea vijiwe mbalimbali katika mitaa ya Mwambani, Mchukuuni, Mwahako, Mwakidila na Mwang’ombe katika kata za Tangasisi na Masiwani kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mkazi na pia kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 27/11/2024.

Akizungumza mara baada ya kuvitembelea vijiwe hivyo amesema kuwa mitaa ndio chimbuko la Amani na Maendeleo kwa Wananchi hivyo ni muhimu kila wananchi wa Tanga Mjini kushiriki.


Related Posts