Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Iran wakutana

WAKATI Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea kugonga hodi kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi na kiteknolojia tayari Iran imemuitikia kwa kuja Tanzania na kufanya uwekezaji wa zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 333.

Akifunga Kongamano la biashara na uchumi la siku nne kuanzia Oktoba 16 hadi leo Oktoba 19,2024 lililozikutanisha Tanzania na Iran, jijini Dar es Salaam, Waziri wa uwekezaji nchini, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa mafanikio ya kongamano hilo ni pamoja na makubaliano ya biashara na uwekezaji wa Miradi 14 yenye thamani ya USD Milioni 333.

Kongamano hilo limeandaliwa na kuratibiwa na TanTrade lilihususekta ya madini mafuta kilimo ujenzi kahawa na nyinginezo ni fursa kubwa kwa nchi ya Tanzania na Iran kuendeleza uhusiano katika biashara na uwekezaji na kuwa na chchu katika ukuzaji wa uchumi

Amesema kuwa Tanzania na Iran imekuwa na mahusiano mema tangu utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Amesema kuwa Tanzania na Iran imekubaliana uwekezaji kwenye takribani 14 yenye thamani ya kiasi cha dola Milioni 333 .

Aidha katika kongamano hilo kampuni mbali mbali za Iran zimesaini Mikataba na kampuni za Tanzania anzania ili kuboresha uhusiano uliopo na kukuza uchumi wa nchi.

“Kupitia utakelezaji wa mikataba hii biashara na uchumi wa nchi zetu utakuwa zaidi kwani limekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na uelewa katika uchumi katika masoko kutambua fursa za biashara na uwekezji zilizopo na kujenga mahusiano ya kibiashara. amesema amesema Prof. Mkumbo

Amesema kuwa Watanzania wamekuwa wanufaika wakubwa wa elimu kutoka kwa watalaam wa hesabu kutoka Iran kama Algebra ambaye ndio Mama wa hesabu naye Mohammad Mussa Algorthsm

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Latifa Khamis amesema kuwa mafanikio ya mkutano huo ni ushirikiano wa kibiashara na diplomasia.

“Imekuwa siku ya mafanikio kwa nchi zetu Mkutano huo uliojadili masuala ya Diplomasia, biashara na uchumi wa nchi kama tunavyofahamu wenzetu wa Iran wamepiga hatua kwenye masuala la chanjo, ujenzi, dawa kilimo sisi tumewaunganisha wafanyabiashara watanzania kuwapa fursa walizokuja nazo wenzetu”

Amesema kuwa licha ya Iran na Tanzania kuwa na uhusiano wa muda mrefu husasan suala la Diplomasia ” kwa sasa sisi Watanzani tunapokwenda Iran tunakwenda bila Visa na kupitia mkutano huu tumesaini mikataba mbalimbali itakayotuimairsha kiuchumi”

Amesema kuwa tayari Tanzania imekubaliana katika mikataba mbalimbali “mkutano huu umeleta tija nyingi kwenye Wizara zetu , Wizara ya Mifugo , Uchukuzi , Wizara ya Afya kwa hiyo mkutano huu umeleta mafanikio kwa nchi yetu na wafanyabiashara mmoja mmoja.

Amesema moja ya mafanikio ni mkataba wa Tantrade na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Iran “wenzetu wa Chemba ya Biashara ya Tanzania (Chember of Commerce) wamesaini mkataba na Chemba ya Biashara ya Iran.

Naye …. wa Iran amesema kuwa makubaliano hayo yanatija kwa nchi zote na kwamba biashara zenye tija zitafanyika.

Amesema kuwa uhusiano wa Iran na Tanzania umeanzia kwenye utamaduni na sasa unakwenda kiuchumi.
“Makubaliano haya yatachochea ukuaji wa sekta binafsi kama ambavyo chemba za Biashara za nchi zetu zilivyokubaliana mikataba uchumi wa nchi zetu utazidi kuimarika”

Amesema kuwa Watanzania hawataingia bila Visa nchini Iran hivyo uhusiano wa kibiashara utazidi kulindwa na kuimarika.
Waziri wa uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Iran baada ya kufunga Kongamano la biashara na uchumi Kati ya Tanzania na Iran. Lililofanyika katika viwanja vya  Mwalimu Nyerere, maarufu kama Sabasaba leo Oktoba 19,2024. Kongamano hilo liliandaliwa na kuratibiwa na TanTrade kwa kushirkiana na ubalozi wa Iran nchini Tanzania.

 

Waziri wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika hafla ya kufunga kongamano la biashara kati ya Tanzania na Iran lililofanyika  kwa siku nne kuanzia Oktoba 16 hadi Oktoba  19 2024 katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo kwenye viwanja vya maonyesho JK Nyerere sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis akizungunza wakati wa hafla ya kufunga kongamano la biashara na uwekezaji  lililomalizika leo Oktoba 19,2024 katika  ukumbi wa Kilimanjaro uliopo kwenye viwanja vya maonyesho vya JK Nyerere (Sabasaba) vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 Kongamano hilo limeandaliwa na Tantrade  kwa kushirikiana na ubalozi wa Iran Nchini Tanzania.

Related Posts