Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wa pili kutoka kushoto akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kituo Maalumu za kurahisisha huduma za Uwekezaji Nchini, Kutoka Kulia ni Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jarida la taarifa za mafanikio ya mwaka mmoja wa TIC, Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na kulia ni Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, na Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha jarida baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza mara baada ya kudindua jarida la taarifa za mafanikio ya Mwaka mmoja wa TIC.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Maalumu kwaajili ya kurahisisha huduma za uwekezaji nchini. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Maalumu cha kuhudumia wawekezaji kitacho wawezesha kupata huduma kwa haraka zaidi pamoja na baahi ya wawekezaji.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amezindua kituo maalumu cha kuhudumia wawekezaji kitacho wawezesha kupata huduma kwa haraka zaidi
Kituo hicho kilichozinduliwa leo Mei 04, 2024 kimejengwa na benki ya Azania kwa lengo la kuokoa muda wa wawekezaji wanaokuja nchini kwaajili ya uwekezaji.
Akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hicho jijini Dar es Salaam, Profesa Mkumbo, amesema kituo hicho ni maalumu kwa kuhudumia wawekezaji katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kusaidia wawekezaji wanaokuja nchini kusajili kampuni kwa haraka zaidi ambapo zoezi la kusajili lilikuwa likichukua muda mrefu.
“Tumeamuwa kufungua kituo hiki ili Mwekezaji akija aweze kusajili kampuni yake hapa na anapotoka awe na cheti cha usajili wa kampuni yake.“ Amesema.
Amesema katika kituo hicho watakuwepo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na wanasheria ambao watasaidia wawekezaji kusajili kampuni zao kwa kuzingatia sheria za Tanzania.
Kwa mujibu wa Prof. Mkumbo amesema kituo hicho kitasaidia kuvutia wawekezaji wengi kutoka nje na ndani ya nchi hivyo wawekezaji hao watatoa fursa za ajira kwa wananchi pamoja na uchumi wanchi kukua.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutekeleza maoni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia wawekezaji wengi zaidi kwa kupitia TIC na kituo hicho kilichojengwa na Benki ya Azania.
“Tupo katika ushindani na kuvutia wawekezaji kutoka duniani na moja ya eneo ambalo wanaangalia ni uharaka wa kuhudumiwa maana yake kwa kufungua kituo cha kusajili kampuni hapa hapa inamanisha kwamba Mwekezaji atapo kuja Tanzania atahudumiwa haraka iwezekavyo na kuaanza shughuli zake mapema.” Ameongeza
Pia ameeleza kuwa Wawekezaji wote wa ndani na nje watahudumiwa kwa usawa na Mwekezaji atakaye ingiza mtaji mkubwa Tanzania atapata huduma maalum.
Kwa Upande wa Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge, amesema kuwa hiyo ni sehemu moja tuu ya utekelezaji wa maeneo ambayo wanaenda kishirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania pia ni kwaajili ya kuunga mkono juhudi za kituo hicho katika kuongeza Wawekezaji Nchini.
“Kipekee tunafuraha sana kushiriki katika uzinduzi wa Kituo hiki kwaajili ya kurahisisha na kuahamasisha uwekezaji nchini na nje ya nchi.
Amesema Mwekezaji atakapofika katika kituo hicho atakutana na huduma zote na kupata huduma za kifedha pamoja na Kufungua akaunti kupitia Benki ya Azania.