RC BABU AAGIZA KUSAKWA WALIOIBA VITABU VYA DAFTARI LA MKAZI.

ROMBO.

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kuiba  vitabu vya majina ya mkazi viwili vilivyoibiwa Oktoba 18 mwaka huu katika kituo cha Josho kijiji cha Kikelelwa kata ya Tarakea Motamburu wilaya Rombo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mpaka sasa linawashikilia watu wanne kwa mahojiano kuhusika na wizi huo ambapo vitabu hivyo vilivyoibiwa vilikuwa vimeshaandikishwa majina ya wananchi 1105 wa kijiji hicho.

Babu alitoa kauli hiyo leo alipotembelea kituo hicho pamoja na Kituo cha Lokoro kilichopo kijiji cha Kikelelwa ambapo watu wasiojulikana walijaribu kuchoma moto ofisi hiyo ya Mtendaji wa kijiji wakijua nyaraka za Daftari la Mkazi zilikuwepo ndani na kupelekea kuchoma moto nyaraka nyingine za serikali.

Alisema kuwa, zoezi la uandikishaji wananchi katika mkoa wa Kilimanjaro limeenda vizuri lakini katika wilaya ya Rombo imeweka dosari na kudai kuwa serikali haitawavumilia wale wote waliofanya vitendo hivo.

“Wapo watu wenye nia hovu wameamua kuiba vitabu vya majina ya wananchi lakini tumeshafanya juhudi ya kuwasiliana na Wizara ya Tamisemi kuomba kwa wananchi ambao walijiandikisha kituo cha Josho na vitabu kuibiwa kuongezewa muda wa zoezi la uandikishaji ili waweze kujiandikisha upya ambapo tumeshakubaliwa hivyo zoezi litaenda mpaka Oktoba 28 mwaka huu” Alisema Babu.


 

Related Posts