Serikali kujenga kituo kipya cha afya Mahuninga

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mahuninga Makifu na Kisilwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo

Diwani wa viti maalumu, Mhe, Shani Richard wa Tarafa ya Idodi akisalimia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mahuninga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akikabidhi Mitungi ya gesi kwa timu za vijana ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mahuninga Makifu na Kisilwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mahuninga Makifu na Kisilwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mahuninga Makifu na Kisilwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na Viongozi wa Chama na Serikali wakati alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Kituo cha Afya Mahuninga.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani amesema Serikali kupitia Benki ya Dunia imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mahuninga.

Ametoa Kauli hiyo wakati wa ziara yake kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Isimani lilopo Mkoani Iringa leo tarehe 19/10/2024 ambapo amefanya mkutano katika vijiji vya Kisilwa Mahuninga na Makifu vilivyopo katika kata ya Mahuninga.

Amefafanua kwamba Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha huduma za afya; huduma za elimu, huduma za maji; ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliaji, ujenzi wa miundo mbinu ya barabara na hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kuweka nguvu katika jitihada za kuchochea maendeleo ili kuimarisha uchumi.

Waziri lukuvi amesema, “Ujenzi wa kitu hicho cha afya utajumuisha ujenzi wa majengo manane mapya, ikijumuisha jengo la wagonjwa wa nje, jengo la maabara, jengo la kinamama na mtoto, jengo la kuhifadhi maiti, jengo la mionzi, jengo la kufulia, jengo la upasuaji na fedha ya ujenzi imeshawekwa kwenye akaunti ya Mahuninga.”

Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutujali sana wanaisimani, tumepata fedha nyingi ndani ya kipindi cha miaka mitatu, ambazo zimeleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika Jimbo la Isimani.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi, ametoa rai kwa wananchi wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kujali itikadi za vyama ili kujenga msingi mzuri wa kuchagua viongozi.

“tunaamini mwakani tutafanya vizuri zaidi katika uchaguzi wa Madiwani wabunge na Rais,” alisema

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mahuninga, Mhe. Benitho Kisogole amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kugharamia miradi ya Maendeleo.

“Ujenzi wa Miundo mbinu ya elimu kwa kipindi cha mwaka 2023-2024 umesaidia sana kuboresha mazingira kufundisha hasa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo na mabweni hivyo ni wajibu wetu kushirikiana ili ujenzi uishe kwa wakati,” alisema

Related Posts