ZIFF, EU WALETA FILAMU TANZANIA BARA 2024

Na. Andrew Chale, Dar es Salaam

TAMASHA la Kimataifa la filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Film Festival-ZIFF) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), Nchini wametangaza rasmi uoneshaji wa filamu katika baadhi ya Mikoa minne ya Tanzania Bara katika Vyuo Vikuu na vituo vya Utamaduni wa Nchi Wanachama hapa nchini program inayofahamika  ZIFF Goes Mainland 2024.

Akizungumza katika utambulisho  rasmi wa ZIFF Goes Mainland 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Joseph Mwale amesema kuwa mwaka huu mpango huo umefadhiliwa na EU kwa baadhi ya Nchi Wanachama kuwasilisha filamu moja hadi mbili zitakazooneshwa kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 21 mwaka huu .

“Mwaka huu tunawashukuru EU kwa udhamini wao katika program ya
ZIFF Goes Mainland 2024, Hii ni sehemu ya tamasha la ZIFF ambapo tunaamini hizi ni jitihada za kulifungua tamasha kuonea maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ZIFF Goes mainland mwaka huu tutakuwa mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mwanza.” Amesema Mwale.

Kwa upande wao baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa EU, wameshukuru Uongozi wa ZIFF kwa kufikia malengo ya kuunganisha tamaduni na desturi za watu wote kupitia filamu sambamba na ukuaji wa sekta hiyo ya filamu hapa nchini.

Aidha, filamu inayotarajiwa kuzindua ZIFF Goes mainland, ni filamu ya Goodbye Jullie.

 

Related Posts