Waziri Mchengerwa ataja mikoa yenye asilimia kubwa ya watu waliojiandikisha hadi Oct 18

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa Leo Oktoba 20, 2024 ametaja Mikoa mitano yenye asilimia kubwa ya watu waliojiandikisha hadi kufikia Oktoba 18, 2024, ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi hilo la uandikishaji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki zoezi la uandikishaji Ikwiriri, Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, Waziri Mchengerwa ameitaja Mikoa hiyo kuwa ni Tanga ambayo imefikia asilimia 101.13 ya lengo la kujiandikisha, Pwani Asilimia 98.74, Mwanza Asilimia 94.09, Dar es Salaam asilimia 86.66 pamoja na Dodoma Asilimia 80.63.

Amesema kuwa Mikoa hiyo mitano pia ni Mikoa yenye idadi kubwa ya watu wenye umri wa kupiga kura kuanzia miaka 18 na kuendelea, ambapo pia hakutakuwa na Simu zitakazoongezwa baada ya jioni ya leo zoezi hilo kuhitimishwa rasmi.

Aidha, amesema kuwa tathmini ya jumla ya zoezi la uandikishaji lililoanza Oktoba 11, mwaka huu itatangazwa Leo usiku majira ya saa sita usiku baada ya kufanyiwa majumuisho.

Related Posts