Daktari Bingwa wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Andrew Foi akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na Kampuni ya Betty World. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza Mafuta ya Ngozi ya Betty Word, Meshack Lutembeka na Mkurugenzi mwenza Bw. Jesse Madauda (wa kwanza kushoto).
Na Mwandishi Wetu.
Jamii imeshauriwa kuacha matumizi holela ya vipodozi bila kufuata mwongozo wa madaktari wa ngozi ili kuepukana na magonjwa ikiwemo kansa ya ngozi.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Andrew Foi wakati wa uzinduzi wa bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na kampuni ya Betty World ambapo pia ameiomba serikali kuendelea kuwekeza katika kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa ngozi ili kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matumizi sahihi ya bidhaa za ngozi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza Mafuta ya Ngozi ya Betty Word, Meshack Lutembeka, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo, Kulia ni Mgunduzi utengenezaji wa mafuta hayo, Dk. Elizabeth Consoli na Kushoto ni Mkurugenzi mwenza Bw. Jesse Madauda.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Betty World akipanga mafuta kabla ya kufanya uzinduzi.
Furaha ya Uzinduzi.
Dk Foi amesema kuwa vipodozi vingi vinavyotumika Afrika zimefanyiwa utafiti kwa wenzetu wazungu … Tanzania hatujabaki nyuma katika kufanya tafiti na kupata vipodozi vinavyoendana na angi ya ngozi yetu. Japo Tanzania madokta wa ngozi ni wachache ila tumejitahidi kusambaa Tanzania nzima.
Amempongeza Dk. Elizabeth kwa kuweza tafiti na kuvumbua vipodozi vinavyoendana na rangi ya Mwafrika jambo ambalo limeweza kuleta utofauti na wavumbuzi wengine.
Daktari Bingwa wa Ngozi na Magonjwa ya Zinaa (Dermatovenereologist) Dk. Cyndy Muliro kutoka nchini Kenya akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa za ngozi, katikati ni Mgunduzi utengenezaji wa mafuta hayo, Dk. Elizabeth Consoli na kulia ni Daktari wa Magonjwa ya Akili Dk Michelle Chapa kutoka nchini Kenya.
Uzinduzi ukiendelea…
Kwa upande wake Dkt Elizabeth Consoli ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Betty world ameeleza kuwa bidhaa hizo zimezingatia utengenezaji wa bidhaa za ngozi zinazoendana na uhalisia wa ngozi ili kuepusha madhara huku akibainiaha kuwa tafiti nyingi zilizofanywa katika kutengeneza bidhaa za vipodozi hazikuhusisha uhalisia wa ngozi za kiafrika
“Elimu ya ngozi kwa sasa inazidi kuendelea mbele na kwa utafiti nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa zimekuwa zikiwatenga watu weusi hivyo basi mimi nimekuja na vipodozi zilizolenga ngozi nyeusi,” amesema Dk. Elizabeth.
Bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kampuni ya Betty World.
Naye mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo Meshack Lutembeka ameeleza kuwa lengo ni kuanzisha kampuni za kizawa zitakazosaidia kulinda afya za watanzania lakini vilevile kuongeza mapato ya fedha za kigeni yanayotokana na kuuza bidhaa zinazozalishwa nchini katika masoko kimataifa.