Waziri Tax apokea kikosi cha jeshi kilichopandisha mwenge Mlima Kilimanjaro

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Stergomena Lawrence Tax October 21,2024 amewasili na kukipokea Kikosi Maalumu cha Jeshi la Wananchi wa JWTZ kilichopandisha Mwenge wa Uhuru pamoja na Bendera ya Taifa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kupandishwa kwa Mwenge huo wa Uhuru pamoja na Bendera ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge huo,Miaka 60 ya Jeshi la Wananachi , Miaka 60 ya Muungano ,pamoja na miaka 25 ya kumbukizi ya Mhasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu alipo aga Dunia.

Hafla ya kupokea kikosi hicho Maalumu imefanyika katika Geti la Marangu, Wilaya ya moshi Mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda,Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu , Patrobas Katambi, Vyombo vya Usalama pamoja na Viongozi wa kisiasa

Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ametoa pongezi kwa kikosi hicho Maalumu kusema kimeonyesha ukakamavu, uzalendo, na umahari katika kufikisha Mwenge huo pamoja na Bendera katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ,Mlima huo wenye Mita za mraba 5895 kutoka usawa wa bahari.

Awali akizungumza katika Hafla hiyo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amesema ametekeleza agizo kwa uangalifu mkubwa alilopewa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama Rais Samia Suluhu Hassan alimkabidhi Mwenge wa Uhuru na Bendera Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, ili Jeshi hilo liupeleke kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge huo.

Oktoba 15, 2024 Kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilianza safari ya kupandisha Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

 

Related Posts