Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika (SADC) lazima ziwe makini sana katika kuuendeleza na kukuza utalii wenye tija na kwa kulitambua hilo GAAB kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameileta safari ya kihistoria itakayokutanisha nchi zaidi ya 16 iliyopewa jina la Live Your Dream Road Tour 2024 hii itakuwa safari ya kwanza ya kihistoria ya kubadilishana utamaduni, kujieleza kwa kutumia sanaa ya uchoraji , na uwezeshaji wa kiuchumi katika kanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Safari hii mahsusi imeandaliwa baada tu ya Zimbabwe kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa owaka mmoja ambapo kijiti hicho cha Urais kilitokea nchini Tanzania .
Lengo kuu la safari hii inayojumuisha zaidi ya kilomita 6,000 ni kuutangaza utalii kupitia nchi za SADC,kuonesha maono ya Kiafrika, ndoto, ubunifu, sanaa, urembo wa asili, urithi, na utofauti wa kila taifa pamoja na kuimarisha ushirikiano na fursa za kiuchumi pia kuongeza ufahamu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), Agenda 2063, na kukuza mipango ya kusaidia maendeleo endelevu ya Afrika. (Cycle 4 SDGs na GAAB)
Kwakupitia progamu hii wanachama 16 na Landrovers zao, kila moja atakuwa na ishara/nembo ya kiwakilishi cha nchi 16 za SADC, huku Landrover ya 17 nembo ya SDG17
Waandaaji wa Event hii hivi sasa wanafanya tathmini ya njia ambazo Landrovers 17 zitapita ili kujionea vivutio mbalimbali mpaka eneo kuu la uzinduzi rasmi ambapo itakuwa ni Marondera Zimbabwe mnamo Oktoba 17
“Safari ya kutimiza ndoto yako na programu ya Sanaa inayoishi” itaanzia nchini Tanzania hadi Zimbabwe Novemba 2024