RC MAKONDA ATANGAZA WIKI YA HAKI ARUSHA



Makonda akizungumza na waandishi wa habari Leo. Mei 3/4/2024 amewaalika wananchi kuleta kero mbalimbali ikiwemo kudhulumiwa au kunyanyaswa kijinsia

Na. Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ametangaza wiki ya Haki
mkoani hapa huku akiwataka wananchi kama yupo aliyedhulumiwa au kufanyiwa ukatili Kufika ofisi ni kwake siku ya Jumatano

Akizungumza na wanahabari jijini Arusha leo, Ijumaa Mei 03.2024 Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ametangaza kuanza kwa siku tatu (3) maalumu za kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa mkoa huo kuanzia Jumatano ya wiki ijayo (Mei 08.2024)

Makonda amewaeleza wanahabari kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na ahadi yake aliyoitoa kwa wakazi wa Arusha Aprili 09.2024 wakati alipowasili kwenye kituo chake cha kazi na kukabidhiwa ofisi na ntangulizi wake John Mongella

Amesema tayari ameandaa taasisi zote za mkoa wa Arusha pamoja na wanasheria wabobezi kwenye mashauri mbalimbali, akiahidi pia kutoa bure wanasheria ili kuwasimamia wananchi watakaokuwa na mashauri yatakayokuwa na uhitaji wa kupelekwa Mahakamani

Zoezi hilo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi litafanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo Mkuu wa mkoa huyo amewahakikishia wakazi wa Arusha na viunga vyake kuendelea kuwa sauti na sikio la wanyonge kwa kuhakikisha waliodhulumiwa na kukandamizwa wanapata haki zao kwa msaada wa ofisi yake.

Related Posts