Kamati ya Bunge yaridhishwa na maelekezo wanayotoa kwa DART

*DART yaahidi kufanyia kazi maelekezo mengine kiutendaji

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI imesema kuwa imeridhishwa maelekezo wanayotoa kwa Wakala wa Mabasi yaendayo (Haraka) yanafanyiwa kazi.

Hayo ameyasema Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Justin Nyamoga wakati Kamati hiyo ilipotembelea Miradi ya Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam amesema kuwa Kamati ilitilia shaka juu ya udhibiti wa mapato lakini DART wametekeleza kuwa kuleta magati janja ambapo abiria atachanja kadi yake na hivyo ukatishaji tiketi utakuwa umekoma.

Amesema kuwa katika wakandarasi wanaojenga kuzingatia masharti ya mkataba na hakuna kuongeza muda kwani kunachelewesha wananchi kupata huduma huku Serikali ikiwa imeweka fedha nyingi katika miradi ya barabara

Nyamoga amesema kuwa mradi wa Mbagala sasa unatakiwa uanze kazi wananchi wamesubiri kwa muda mrefu ikiwa ni pamojà na kutafuta watoa huduma wa uhakika wa kutoa huduma ya usafirishaji abiria.

Aidha amesema Kamati hiyo ni kuona kile ambacho wanachokiona kilete matokeo chanya pamojà na kuwa watoa huduma wanakwenda kutoa huduma hiyo kwa viwango vyenye ubora.

Nae Naibu Waziri wa TAMISEMI Zainabu Katimba amesema kuwa wakandarasi waafanye kazi kwa mujibu wa mkataba na kusipo vizingizio kutokana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameetoa fedha nyingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Katimba amesema kuwa kama wasaidizi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kusimamia kwa vitendo kuonyesha kile anachokiamini kinafanyiwa kazi hivyo hataachwa mtu anayetaka kumuangusha Rais.

Naibu Waziri Katimba amesema kuwa Serikali imetoa fedha nyingi katika miradi ya BRT hivyo lazima huduma zinazohitajika Kwa wananchi lazima wapate.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa wameyapokea maelekezo ya Kamati kwa kwenda kufanyia kazi.

Amesema kuwa walichojifunza katika mradi wa awamu ya kwanza hawataki itokee kwani mradi utakuwa unaanza kwa kuwa na mabasi yanayoendana na mahitaji ya abiria.

Amesema watoa huduma wameshapatikana ambao wameshachukua michoro Kwa ajili ya mabasi yatayotoa huduma ya usafirishaji ikiwemo Gerezani hadi Mbagala.

Kihamia amesema mabasi ya mradi huo ni tofauti haiwezekani ukachukua basi aina yeyote likafanya kazi kinachofanyika ni kuchikua michoro na kisha kwenda kutengeneza mabasi hayo.
 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kudumu ya TAMISEMI Justin Nyamoga akizungumza na waandishi wa habari wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

Naibu Waziri wa TAMISEMI Zainabu Katimba akizungumza na waandishi kuhusiana mradi wa Mabasi yaendayo Haraka wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI ilipotembelea Ujenzi wa mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Dkt.Athumani Kihamia akizungumza na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI wakati Kamati ilipotembelea Ujenzi wa mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Dkt.Athumani Kihamia akizungumza na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI wakati Kamati ilipotembelea Ujenzi wa mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Dkt.Athumani Kihamia akizungumza kuhusiana na mageti janja yatayotumika katika kutoa huduma ya malipo katika vituo vya mabasi yaendayo haraka wakati kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI  ilipotembelea Ujenzi wa mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

picha ya pamojà ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI ilipotembelea Ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka

Related Posts