Vikundi vya ulinzi shirikishi zingatieni maadili ya Kazi

Vikundi vya Ulinzi Shirikishi Kata ya Ngara Mjini Wilaya Ngara Mkoa wa Kagera vimetakiwa kuzingatia Sheria kipindi cha utekelezaji wa majukumu yao huku akiwataka kuwa mfano mzuri Kwa jamii.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo wakati akitoa elimu Kwa vikundi hivyo ambapo amewataka kufuata sheria za mwenendo wa Makosa ya Jinai akiwakumbusha *kifungu cha 21 kifungu kidogo cha kwanza* cha ukamataji salama.

Mkaguzi Olipa amewataka kutambua kuwa vikundi vya ulinzi Shirikishi ni Miongoni mwa Wadau wa karibu wa Jeshi la Polisi katika masuala ya Ulinzi ambapo amewasisitiza kufanya kazi Kwa weledi Mkubwa ili kuzuia malalamiko na masononeko kwa wananchi.

 

Related Posts