Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ndositwe Haonga amefungua mkutano wa 19 wa Mamlaka za Mapato katika nchi za Afrika Mashariki wenye lengo la kushirikishana mbinu na mikakati mbalimbali ya maadili ili kupambana na vitendo vya rushwa vinavyopelekea upotevu wa kodi.