Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Husna Sekiboko (MB), ametoa wito kwa serikali kuijengea uwezo Bodi ya Filamu nchini ili iweze kushindana katika soko la kimataifa.
Akizungumza katika kikao cha kamati kilichofanyika leo, 23 October 2024 Mheshimiwa Sekiboko alisisitiza umuhimu wa kuimarisha utendaji wa bodi hiyo ili kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa.
Amesema kuwa uwezeshaji huo utaongeza ubora wa filamu zinazozalishwa nchini na kuvutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje na kuitangaza nchi kimataifa.
Kikao hicho kilijadili changamoto mbalimbali zinazokabili Bodi ya Filamu na mikakati ya kuzitatua ili kuimarisha sekta ya filamu.