TASAC yawapiga msasa Kikosi cha Polisi cha Wanamaji

*Yataka ushirikiano wa karibu katika udhibiti wa vyombo vidogo vya majini

Na Chalila kibuda ,Michuzi TV

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa mafunzo kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Polisi cha Wanamaji katika masuala ya usimamizi wa vyombo vya majini.

Akizungumza wakati wa utoaji wa Mafunzo kwa Jeshi la Polisi Kikos cha Wana Maji jijini Dar es Salaam ,Afisa Mkaguzi na Msajili wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Gadaf Chambo amesema kuwa kuna vyombo vidogo vinasafirisha abiria kutoka Feri kwenda kigamboni ni kosa kisheria.

Amesema katika eneo la Feri ni hatari kufanya vyombo vidogo kusafirisha abiria kutokana na meli zinaweza kuruhusiwa na kusababisha kupinduka.

Amesema kikosi cha wana maji wajubu kusimamia vyombo vidogo kutofanya huduma hiyo.

Chambo amesema kuwa vyombo vidogo vidhibitiwe kutokana baadhi yao wanafanya biashara za haramu ikiwemo dawa za kulevya,uvuvi kwa kutumia mabomu.

Aidha amesema kuwa TASAC ina jukumu ya kuvisimamia vyombo vya majini hivyo Askari vyombo hivyo vikionekana na abiria sheria ziko wazi kuvichukulia hatua.

Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi Wanamaji Shomari Mashaka amesema kuwa wanashukuru kwa mafunzo hayo katika kwenda kutekeleza majukumu ya kusimamia katika kuepuka na athari ambazo zinaweza kujitokeza.

Mashaka amesema elimu hiyo TASAC iendelee kuwa utaratibu wa mara kwa mara katika kujengea uwezo na kubadilishana taarifa katika matukio ya polisi tunayokutana nayo.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji Fatuma Msuya amesema katika mafunzo hayo kuna kitu amekipata cha kuweza kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu.

Amesema kuwa wanakutana na matukio katika kutengeneza mashitaka wanashindwa kujua lakii sasa kwa elimu hiyo wataweza kutengeneza mashtaka ambayo yapo kwamujibu wa sheria.
 

 Afisa Mkaguzi na Msajili wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Gadaf Chambo akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa Polisi wa Wanamaji  kuhusiana udhibiti kwa watu wanaokiuka taratibu wa uendeshaji wa vyombo vya majini jijini Dar es Salaam.
 

Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji Shomari Mashaka akizungumza kuhusiana na umuhimu wa mafunzo hayo kwa askari ,jijini Dar es Salaam.

 

 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi Wanamaji /Mkuu wa Upelelezi Kikosi cha Wanamaji Fatuma Msuya akizungunza kuhusiana na umhimu wa mafunzo yatavyosaidia kuimarisha utendaji kwao jijini Dar es Salaam.
 

Picha ya pamoja kati ya TASAC  na Kikosi cha Polisi Wanamaji  mara baada ya kuhitimsha mafunzo ,jijini Dar es  Salaam.

Related Posts