TCRA na TAMWA wamekuja na hii kwa waandishi wa habari

Leo 24 Oktoba 2024 – Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wamezungumza na waandishi wa Habari kutangaza kuzisogeza mbele Tuzo za ‘Samia kalamu Awards’ ambazo walizindua tarehe 13 Oktoba 2024, ikiwa ni ushiriki wa wanahabari katika tuzo hizo zenye kaulimbiu “Uzalendo Ndio Ujanja.”

Wakiongea na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa DKT Rose Reuben ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji – TAMWA akiwa na DKT Jabiri Bakari Mkurugenzi TCRA wamesema utaratibu wa kujiandikisha na kuwakilisha kazi katika Tuzo hizo za Samia Kalamu Awards umesogezwa mbele hadi Octoba 30, 2024 na hapo awali, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ilikuwa ni Oktoba 26, 2024.

Hata hivyo, uamuzi huu wa kuongeza muda umechukuliwa ili kutoa nafasi kwa wale valiokutana na changamoto za kiufundi, ikiwemo kushindwa kupandisha kazi mitandaoni, kutokana na matatizo ya mtandao na changamoto nyingine, Tuzo hizi zitatolewa kwa wanahabari wa Kitanzania, zikiwa na lengo la kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani, kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni, ili kuchochea uandishi wa makala za kina zinazozingatia maendeleo, uwajibikaji, mila na tamaduni pamoja na kujenga chapa na taswira ya nchi.

#MillardayoUPDATES

Related Posts