MALIMA AKABIDHI GARI RUWASA WILAYA YA MALINYI

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
MKUU  wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amekabidhi gari kwa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Malinyi katika hafla iliyofanyika ofisini kwake.
Katika Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba pamoja na watumishi wa RUWASA Mkoa.

Malima amesema gari hilo litasaidia kuboresha huduma za usafiri kwa watumishi wakati wa kukagua miradi ya maji vijijini.

“Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora za maji, hasa katika maeneo yanayokabiliwa na changamoto za usafiri”. Amesema Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba, ameishukuru serikali kwa kutoa gari hilo, akieleza kwamba litasaidia kuongeza ufanisi wa kazi kwa watendaji na kufika maeneo ya miradi ya maji.
Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Sospeter Lutonja, amesema gari hilo litawawezesha wahandisi na wafanyakazi wa RUWASA kufika haraka katika maeneo yanayotekeleza miradi ya maji
Kutolewa kwa gari hili ni sehemu ya juhudi za serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za maji safi na usafi mijini na vijijini, lengo likiwa kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji ifikapo 2025.

Related Posts