Mchezo wa Makachu ni fursa ya kuitangaza Zanzibar kimataifa :Rais Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Mchezo wa makachu umekuwa fursa nzuri ya kuitangaza Zanzibar kimataifa .

Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 24 Oktoba 2024 alipofika Bustani ya Forodhani Kuangalia Mchezo huo ambao umekuwa maarufu na kuvutia wenyeji na wageni wengi wanaokuja nchini.

Aidha Rais Dk ,Mwinyi amewasisitiza Vijana wanaopiga makachu kuuendeleza Mchezo huo kwani umekuwa ukitizamwa na kufuatiliwa na watu wengi sehemu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa Vijana wa makachu walitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk, Mwinyi kwa kuonesha mabango ya mafanikio ya Serikali katika sekta mbali mbali.

Tukio hilo ni muendelezo wa shamra shamra za kupongeza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais Dk.Mwinyi.

 

Related Posts