Ziara ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi RUWASA yazaa matunda Kagera

Kupitia ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Mhandisi Lucy Koya aliyoifanya Mkoani Kagera kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo tayari imeanza kuonyesha manufaa kwa baadhi ya wananchi Mkoani humo.

 

Akiwa Mkoani Kagera akiongozana na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Kagera mhandisi Warioba Sanya sambamba na watumishi wengine wamefanikiwa kutembelea miradi mbalimbali na kuongea na watumishi wa jumuiya za watumiaji maji katika Wilaya za Missenyi,Bukoba,Kyerwa na Muleba

 

Kwa upande wa wa Wilaya ya Kyerwa Mhandisi Koya amewaagiza RUWASA kuwachimbia kisima cha maji wananchi wa kata ya Songambele ambao wamekuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu.

 

Pia akiwa Wilayani Muleba amefika kwenye mradi wa maji wa Bushagara-Kamachumu ambao umefikia asilimia 94 ukigharimu zaidi ya milioni mia tisa na tayari ushaanza kutoa maji na unatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya elfu nne.

 

Kupitia mradi huo ameipongeza RUWASA Mkoani Kagera kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maji huku akiwataka wananchi kutunza miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu

 

Related Posts