Zaidi ya Bill 1 zakusanywa kujenga wodi ya mama na watoto,mfumo wa maji taka na kisima cha kuhifadhia maji

Zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia moja (1,100,000,000) zimekusanywa na wadau mbali mbali kwa lengo la kusaidia ujenzi jengo la ghorofa moja la wodi ya mama na mtoto na wodi ya vitanda 25, mfumo wa maji taka, kisima cha kuhifadhia maji lita 400,000 ambapo kwa sasa kuna kisima cha lita laki 1, kwa ujumla utanuzi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.2

 

Zoezi hilo la uchangiaji limefanyika katika ukumbi wa mlimani city huku likiongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora George Simbachawene ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani

 

#MillardAyoUpdates.

Related Posts