Samaki Samaki ilivyosheherekea miaka 17, ni Burudani kwa kwenda mbele

Mgahawa maarufu wa Samaki Samaki, jijini Dar es Salaam, ulitimiza miaka 17 tangu ulipoanzishwa rasmi mwaka 2007. Mgahawa huu, unaomilikiwa na mfanyabiashara maarufu Carlos Bastos, maarufu kwa jina Kalito Samaki, umekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya chakula na burudani nchini Tanzania. Kupitia mafanikio hayo, mwaka 2020, ulizalisha mgahawa mwenza unaoitwa *Kukukuku*, ambao pia jana ulitimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake.

Kalito’s Way Group (KWG), inayomiliki migahawa ya Samaki Samaki, Kukukuku, na Wavuvi Kempu, imeleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya burudani na chakula nchini, ikijulikana kwa mtindo wao wa kipekee wa *house style* na uwepo wa DJs katika maeneo yao. Pia wamejipambanua kwa ubunifu wa majina na menyu za kipekee zinazopatikana kwenye migahawa yao, hali inayowafanya kuwa kivutio kwa wateja wanaotafuta ladha na uzoefu tofauti.

Katika kuadhimisha mafanikio yao, hafla hiyo ilipewa majina rasmi – *El Anniversario* kwa Samaki Samaki na *Fantastic 04* kwa Kukukuku. Sherehe hizo zilifanyika kwenye eneo la brunch la Samaki Samaki lililopo Mlimani City, ambapo kulikuwa na burudani za moja kwa moja na maonesho yaliyohudhuriwa na wasanii maarufu, viongozi wa makampuni, na wageni kutoka sehemu mbalimbali za jiji.

 

Wageni waliburudika na chakula cha kisasa na muziki, huku uzoefu mpya wa huduma ya VIP uliopewa jina “NEW VIP, KWA MADON” ukiwavutia wengi, hasa katika brunch ya Mlimani City. Samaki Samaki inajivunia miaka 17 ya ubunifu na mapinduzi yaliyowaleta karibu zaidi na wateja wao kupitia huduma za kipekee na zinazozidi kuboreshwa kwa ajili ya kufanikisha matamanio yao ya burudani na ladha.

Related Posts