Picha: GSM achangia Milioni 200 kupitia GSM Foundation katika tukio hili DSM

Rais wa kampuni za GSM Group of Companies Mr. Ghalib Said Mohammed jana akiambatana na Mkuu wa @gsmfoundationtz Ms. Faith Gugu na Mratibu wa GSM Foundation Mr. Julius Ndakoha, ametoa ahadi ya kuchangia kiasi cha TZS milioni 200 kupitia GSM Foundation na tani 100 za mifuko ya simenti kupitia Young Africans SC kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwatunza, kuwahudumia na kunufaika na mafunzo na busara za wazee cha @petra_elderly_centre

GSM Foundation pamoja na Young Africans SC wameunga mkono harambee hiyo ya kuchangia kituo hicho cha wazee ambacho muasisi wake ni Mh. Dkt. Stegomena Tax, iliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa the SuperDome , na kuhudhuriwa na mgeni Rasmi Rais Mstaafu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wadau wa Taasisi mbalimbali.

Related Posts