Klabu ya Manchester United imemtimua meneja wake, Erik ten Hag baada ya miaka miwili ya kuiongoza klabu hiyo. Inaripoti Mitandao ya KImataifa, Manchester, England … (endelea).
Mholanzi huyo alielezwa kuhusu uamuzi uliofikiwa na bodi ya klabu hiyo leo ikiwa bado wanaugulia na kipigo cha mabao 2-1 walichokipata jana mchana kutoka kwa West Ham.
Ruud van Nistelrooy, aliyepata kuwa mchezaji wa timu hiyo miaka ya nyuma ndiye atakaimu nafasi hiyo who joined katika kipindi cha mpito cha kusaka meneja mwingine.
Kipigo cha 2-1 ilichokipokea jana kimeifanya United kushika nafasi ya 14 katika msimamo wa timu 20 zinashiriki ligi kuu England na mpaka sasa imeshinda mechi tatu kati ya tisa ilizocheza.