AQRB YATARAJIA KUONESHA UJUZI MPYA NA TEKNOLOJIA ZA KISASA KWENYE MKUTANO WA MWAKA

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi (AQRB) inatarajia kufanya mkutano wao wa mwaka ambao utafanyika tarehe 29-30 Oktoba 2024 ambapo umelenga kutoa  taarifa ya bodi katika nyanja ya mafanikio pamoja na changamoto zilizo jitokeza katika kipindi Cha mwaka mmoja.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba  28,2024 Msajili AQRB Mbunifu Majengo Edwin Nnunduma amesema katika mkutano huo watautumia piakutoa mafunzo endelevu kwa wataalamu wa masuala ya ujenzi.

“Mafunzo hayo endelevu ya wataalamu yatafanyika kwa njia mbili moja ni maonesho kutakuwa na mabanda ya bidhaa na vifaa vya ujenzi,na pili kutakuwa na wataalamu”Amesema.

Aidha Nnunduma amewaalika wananchi na wadau katika sekta ya ujenzi kuhudhuria katika mkutano wao ambapo watapata fursa yakujionea na kuzitambua  Teknolojia za kisasa ambazo zikitumika katika ujenzi zinaokoa gharama pamoja na muda.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Dkt.Boniphace Bulamile ameeleza kuwa kwenye mkutano huo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mmkoa wa Dar es Salaam akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko.

Aidha Bulamile amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwasajili wataalamu wa ujenzi ambapo wataalamu wao wanazingatia aina ya jengo la kujengwa kulingana na ardhi ya eneo husika.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam ambapo umebeba kauli mbiu isemayo MABADILIKO YA MBINU NA TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA UJENZI TANZANIA

Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Dkt.Boniphace Bulamile akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2024 kuelekea Mkutano wao wa mwaka ambao utafanyika tarehe 29-30 Oktoba 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi (AQRB) Mbunifu Majengo Edwin Nnunduma akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2024 kuelekea Mkutano wao wa mwaka ambao utafanyika tarehe 29-30 Oktoba 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Usajili na Mafunzo Mashaka Bundala akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2024 kuelekea Mkutano wao wa mwaka ambao utafanyika tarehe 29-30 Oktoba 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Related Posts