Wananchi wa Kawaida EAC Kuwezeshwa mifumo rahisi ya Fedha Mtandao

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdallah Makame asema wananchi wengi wa kawaida wa nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki wakiwezeshwa kutumia mfumo wa Fedha kwa Mtandao wataweza kujinasua katika umasikini na kuboresha maisha yao.

“Tunaangalia hayo kwani wenzetu wengi wananchi wa Kawaida wanataka kujinasua na kujikwamua kutoka katika umasikini na waweze kuboresha maisha yao lakini mfumo wa kifedha umewatenga, lengo la jukwaa hili ni kubadilishana Mawazo na kuangalia namna Ya kuboresha mifumo ili watu wengi washiriki katika mifumo rasmi ya kifedha ya Kidigiti” amesema Makame.

 

Akizumgumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la Kisera za uchumi wa kidigitali lililowakutanisha watafiti mbalimbali wakiwemo wadau wa taasisi za fedha Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame amesema jukwaa hilo linalenga kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuwasaidia wananchi wa kawaida katika ukanda wa Afrika Mashariki kutumia mfumo wa fedha kwa njia ya mtandao kukuza kipato chao.

Jukwaa hilo limeendeshwa na Taasisi ya utafiti ya afrika ya uchumi na kudhaminiwa na Bill & Melinda Gates Foundation

Mgeni Rasmi katoka Kongamano hilo ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Abdallah Makame.

Related Posts