IFM yatwaa tuzo ya mshindi wa kwanza katika Wiki ya Huduma za Fedha

*Yaweka mikakati ya kutoa elimu ya fedha kwa vikundi

Na Mwandishi Wetu 

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IMF) kimetwaa tuzo ya mshindi wa kwa kwanza katika kilele cha Wiki ya Huduma za Fedha.

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa Tuzo na Cheti Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho Dkt.Grace Kazoba alisema kuwa ushindi huo umetokana na kujipanga katika utoaji wa elimu kuhusu masuala ya fedha.

Amesema kuwa ushindi huo ni kielelezo cha kujipanga zaidi katika masuala ya fedha kutokana na Chuo ndio eneo lake kubwa katika kutoa elimu kwa wanafunzi ambao wanakuwa mabalozi katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa katika utoaji elimu katika wiki ya huduma za Taasisi za Fedha walikuwa na maeneo mawili ambayo ni kutoa elimu ya masuala ya fedha ikiwa ni ubia na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na eneo la pili kuhusiana na masuala ya Hisa.

Amesema kuwa juu masuala ya fedha wananchi wengi hawana elimu ya fedha na kuwa changamoto katika mikopo katika taasisi za fedha.

Dkt.Grace amesema eneo la pili kufundisha soko la hisa linahitaji elimu ambapo wanafunzi na jamii wakiweza kujua watakuwa wamejikwamua kiuchumii.

Aidha amesema kuwa katika mipango mikakati wameweka program za watu kusoma kwa muda mfupi kuanzia siku kwa vikundi au mtu mmoja mkoja ili kwenda kufundisha kwa vitendo masuala ya fedha na kuwa jamii yenye uelewa wa masuala ya fedha.
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt.Grace Kazoba akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza kutoka kwa Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja  wakati wa hafla ya kufunga wiki ya huduma za fedha iliyofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe jijin

 

Matukio katika picha ya Tuzo na Cheti kwa IFM kwenye Wiki ya Huduma za Fedha ,jijini Mbeya.

Related Posts