WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe. Pindi Chana amehudhuria hafla ya uzinduzi wa Asasi ya kichina iliyofanyika Mjini Mafinga Wilayani Mufindi akiwa Mgeni rasmi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri Chana amesema “Mnafanya jambo jema kuwekeza kupitia Viwanda katika maeneo mengi hapa Nchini, Tanzania na China Tumeendelea kuwa na mahusiano mazuri kwa muda mrefu yaliyoanzishwa na Waasisi wetu Mwalimu Nyerere na Mao tse tung hivyo hatuna budi kuendelea kudumisha haya mahusiano”.
Amesema Waziri Mhe. Chana.
Pamoja na hayo Mhe. Chana ameongezea kwa kusema kuwa mahusiano baina ya Nchi Hizi mbili Tanzania na China yawe na manufaa makubwa katika kukuza Uchumi pamoja na kuwezessha Ajira kwa Vijana.
Asasi hiyo ya Kichina inalenga kujenga mahusiano thabiti yenye kuleta sauti ya pamoja kati ya Tanzania na China kupitia uwekezaji na Biashara.