Rais Mwinyi awasili nchini Qatar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Doha,Qatar ambapo anatarajia kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa kutimia miaka Thelathini ya Familia Duniani utakaofanyika tarehe 29 hadi 31 Oktoba 2024 nchini Humo.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad Rais Dk.Mwinyi na ujumbe wake amepokelewa na viongozi waandamizi wa Qatar wakiongozwa Mhe. Youssef Al Harami na Balozi wa Tanzania nchini Qatar,Balozi Habibu Awesi Mohamed.

Ushiriki wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika Mkutano huo mkubwa wa Kimataifa utaongeza chachu ya Ustawi wa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Related Posts